TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 17 November 2014

EDWARD LOWASSA MMH...MASTAA KUMFANYIA BONGE LA PATI!

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper. Chanzo makini kilichopo ndani ya kamati ya wasanii hao wa Bongo Movies, kitendo cha Taasisi ya Twaweza kutangaza kuwa Lowassa anaongoza na kuwagaragaza makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwao ni ishara tosha ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao. 

SIKU chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangazwa kuwa anaongoza katika kinyang’anyiro cha urais 2015, mastaa mbalimbali wanaomuunga mkono wameandaa mkakati wa kumfanyia sherehe ya kumpongeza. 

“Mastaa wa Bongo Movies wanaomuunga mkono Lowassa wameandaa bonge la pati la kumpongeza Lowassa na siku hiyo watakula, watakunywa maana mipango yao tayari wanaona inakwenda vizuri na hakuna mtu ambaye anaweza kumuangusha katika chama hicho,” kilisema chanzo bila kutaja lini na wapi watakapofanyia sherehe hiyo

No comments:

Post a Comment