TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday 9 October 2013

ZINGATIA MAMBO HAYA (7) KATIKA BIASHARA YAKO.


Wakati mwingine huwa tunajiuliza ni namna gani au ni mikakati gani tutumie ili kukuza biashara, ukweli ni kwamba licha ya kuwa na ushindani mkubwa wa kibiashara bado wewe kama mfanyabiashara una uwezo mkubwa wa kubadilisha na kukuza biashara yako.Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia unapotaka kufungua au kukuza biashara yako.
Learn How to Impliment Direct Marketing Into Your Business and Boost Your Profits From This Video.

      1.Thaminisha bidha unazo uza.
Iwe biashara ndogo au kubwa bidha unazouza ni muhimu ziwe zenye ubora na muonekano mzuri utakaomvutia mteja.Watu hupenda vitu vizuri,bora na vinavyodumu hivyo ni vema utengeneze bidha zenye ubora na thamani Good businessman serves quality products to his customers.’’

  2.Fanya biashara ya kipekee.
Fikiri na kuwa mbunifu katika kubuni na kuibua biashara. Mfano kama mahali unapotaka kufanya biashara kuna huduma za M-PESA, AIRTEL MONEY au biashara nyingine maarufu wewe pia unaweza kufanya na vilevile ukaongeza biashara yako binafsi kwa kubuni na kuibua biashara mpya tofauti na wengine. Kufanya hivyo utaweza kuwa mfayabiara wa kipekee kwa kuwa na huduma nyingi watu wanazohitaji.

3.Pata ushauri kwa watu waliofanikiwa kibiashara.
Unapokuwa katika wakati mgumu wa kutatua matatizo yako ya kibiashara au unapokuwa na utata katika kufanya maamuzi sahihi ya namna ya kuanza biashara ni vizuri utafute ushauri kutoka kwa watu ambao tayari wamefanikiwa katika biashara kama yako.Pia unaweza kutafuta watu wa kukufundisha jinsi ya kufanya biashara yaniBusiness Mentors” ambao watakusaidia kupata ujuzi sahihi na kukupatia maarifa kuhusu biashara.

 4.Uza bidha kwa bei inayokubalika na wengi.
Wateja hupenda kununua vitu kwa BEI POA! hivyo ni muhimu kujua utauza bidha zako kwa bei kiasi gani. Hapa si maanishi uuze bidha kwa bei rahisi bali uzingatie bei ambayo wateja wengi wanaweza kukidhi. Mfano; Unataka kufanya biashara ya kuuza keki, gharama ulizotumia kutengeneza na kuandaa keki ni shilingi 2500/= kwa keki moja badala ya kutaka faida kubwa kwa kuuza shilingi 5000/= unaweza kuuza kwa shilingi 3500/= ambayo utapata faida ya shilingi 1000/= mathalan vilevile utapata wateja wengi na kuuza keki nyingi kuliko utakopo uza kwa bei kubwa ambayo utapata wateja kidogo.
      5.Tangaza biashara yako.
Biashara ni matangazo hivyo ukitaka biashara yako ikue kwa kupata wateja wengi huna budi kuitangaza ili watu waifahamu. Siku hizi kuna njia nyingi za kutangaza biashara ikiwemo kupitia wavuti, radio, runinga au hata mabango.Kumbuka tumia maneno mazuri ya kuvutia na kushawishi wateja.
  


      6.Jiamini na usikate tamaa katika biashara.
Kuna wakati unapoanza biashara mambo huwa mabaya hivyo ni vema ujiamini na utafakari ni wapi umekosea au ni nini cha kufanya ili uboreshe biashara yako.Hakuna mafanikio ya haraka hivyo uvumilivu na ukakamavu ni muhimu sana katika kukuza biashara yako.

      7.Fanya biashara uipendayo.
Naamini kama mtu atafanya kazi aipendayo basi ataifanya kwa uhodari na kupata mafanikio makubwa, swala hili ni muhimu pia katika kuamua ni biashara gani unapenda kuifanya. Mfano kama wewe umesomea fani ya uhandisi wa majengo ni vema ukafanya biashara kwa kuanzisha biashara yako ya mambo ya  ujenzi. Kama unapenda kupika fungua mgahawa au fanya kazi inayohusiana na fani unayopenda. Maendeleo na mafanikio makubwa ya kazi yeyote ile huletwa kwa kufanya kazi unayoiridhia na kuipenda.

Hayo ni mambo machache na ya kawaida ya kuzingatia katika biashara yako, kuwa na ndoto kubwa ya kufanikiwa kibiashara ni vizuri lakini pia penda kujua mengi kuhusu mahusiano ya biashara na wateja kwani biashara ni watu hivyo kuwa makini kwa kila hatua unayopiga kibiashara ili kuepuka hasara.
 
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako.
 
 
 
BY kamotta

No comments:

Post a Comment