Hivi ndivyo Barabara ilivyokuwa kabla
Waandishi wa Jiji wakiwa wamefika kuwashangaa wenzao wakiwa wanafanya kazi ya kutejenga Taifa , wa pili kutoka kushoto ni Mwandishi wa Habari wa Bomba Fm Radio Richard Kamanga aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza Barabara hiyo akiongea nao.
Baadhi ya wamachinga na wananchi wa eneo hilo aibu zikiwa zimewashuka na kuamua kushirikiana na Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm Radio na Mbeya yetu Blog kuendelea kutengeneza njia hiyo
Waandishi wa Jiji wakiahidi kuleta kifusi kwa ajili ya kurekebisha Barabara hiyo
Wachina wakiwa wamefika eneo la tukio na kuahidi kuwa nao wataongeza nguvu katika ujenzi wa Barabara hiyo
Mchina akipata maelekezo juu ya Barabara hiyo
Hii ndio kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Mbeya yetu Blog sambamba na Bomba Fm Radio .
Picha na Mbeya yetu
********************
Wakati kazi ikiendelea baada ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuingia Mitini, na tukio hili kuripotiwa muda mchache uliopita kupitia Mtandao huu na Bomba Fm Radio huku waandishi hao wakiendelea ya kujenga Taifa ndipo Ghafla waandishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walipoweza kufika na kuwashangaa wenzao wakiendelea kupiga kazi na baada ya kuona aibu waliamua kuahidi kuleta kifusi kwa ajili ya matengenezo ya Barabara hiyo.
Nao Baadhi ya wamachinga wapenda maendeleo waliweza kujitokeza kwa ajili ya kuwaunga mkono waandishi wa habari walioanzisha kazi hiyo na kuwasaidia kazi inayo endelea ya ukarabati wa kipande hicho cha barabara. Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
Hii ndio Hali halisi ya Barabara ya Block T ambapo imeharibika na kusababisha Dala dala kutaka kugomea kupita katika Eneo hilo kuhofia kukwama.
Hii ni sinto Fahamu ambapo wakati waandishi wa Habari waliojitolea kurekebisha Barabara hiyo wakiendelea na kazi ya kuziba mashimo hayo , watumishi wa Jiji wenyewe walikuwa ndani ya Gari lao wamefunga vioo na kushangaa kinacho endelea bila kuonesha ushirikiano wowote na Baadae waliondoka, Jambo ambalo limewashangaza watu wengi, Huku wakiwa wameahidi wangerekebisha Muundombinu huo.
Mmoja ya Gari dogo likiwa limesimama baada ya kuona kuwa Njia ni mbaya
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Bomba Fm wakishirikiana na Mbeya yetu Blog wakianza kuchukua Kifusi na Kuziba Barabara hiyo.
Msimamizi Mkuu na Mwandishi wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango akiwa anaendelea na kazi ya kuziba eneo hilo lililoharibika
Hali halisi ya Njia hiyo
Mmoja wa wasukuma Mkokoteni akiwa amejitosa kupita katika tope na kuendelea na safari , kutokana na kwamba alikuwa hana Njia nyengine zaidi ya hiyo
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm Radio wakiendelea na Kazi
Kazi imepamba moto ambapo waandishi wa Habari kutoka Bomba FM wakiwa wamekomaa kuendelea kuziba mashimo katika barabara hiyo iliyo haribika kwa kiwango kikubwa huku wakazi na wafanya biashara wa eneo hilo wakiwa wanatazama bila kufanya juhudi zozote za kutengeneza, lakini wakisikia kuna mgomo wanakuwa wakwanza kwenda andamana na shughuli za kijamii kama hizi kuzisusia
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi ili kupisha Magari yaanze kutumia Njia hiyo huku Wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo wakiwa wanapaangalia tu, na Jiji kufika hapo na gari lao bila kufanya kitu chochote
Kazi ikiwa inaendelea kwa kasi kubwa
Kila mmoja yupo bize
Kazi inaendelea kusonga mbele Picha na Mbeya yetu
********************************
Mbeya yetu Blog kwa ushirikiano mkubwa kabisa na Bomba Fm Radio (elimisha burudisha) waamua kurekebisha kipande cha barabara inayo tumika kupitia daladala zinazo toka uyole kuelekea s/kuu kipande hicho kilichopo Block 'T'
Ushirikiano huo wa vyombo hivyo viwili vya habari umekuja baada ya madereva wa daladala kutaka kuweka mgomo kwaajiri ya kipande hicho cha barabara kuwa kibovu kinachokuwa ni tatizo kwa daladala hizo.
Wakati tukio hilo la ukarabati likiendelea Halimashauri ya Jiji la Mbeya wamefika na kuwashangaa tu bila hata kuchukua hatua yoyote na hatimaye kuondoka vivyo hivyo, wamachinga wa maeneo hayo pia wamegoma kutoa ushirikiano wakati wakiambiwa kuhusu masuala ya mgomo huwa mbele kwaajiri ya kuchafua amani.
Bomba Fm Radio na mbeya yetu Blog wamechukua hatua hiyo ili kuepusha migomo isiyo kuwa yalazima kutokana na kupenda amani na kuwajali watanzania ambapo Halimashauri ya Jiji ilitoa ahadi ya kutengeneza lakini mpaka sasa haijaweza kufanya jambo lolote kuhusiana na sehemu hiyo.
Mtazamo : Halimashauri ya Jiji la Mbeya mnapo wahamisha watu kutoka sehemu moja kuelekea sehemu nyingine tunaomba muhakikishe mmewawekea miundombinu ya kutosha ili kuepusha mambo machache yanayo weza kuwa ni tatizo kwa wananchi
No comments:
Post a Comment