1.0 UTANGULIZI
Pamoja na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.
Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-
- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
- Taasisi ya Mifupa MOI;
- Hospitali ya Bugando.
- Magonjwa ya Moyo
- Magonjwa ya Wanawake
- Magonjwa ya Watoto
- Upasuaji na
- Mabingwa wa Dawa za Usingizi.
LENGO LA KUANZISHA MPANGO HUO:
Lengo la kuanzisha mpango huo ni:-
- Kuwapeleka Madaktari Bingwa katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa madaktari bingwa na kuwatumia wataalamu hao wachache kitaifa;
- Kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma za madaktari bingwa katika miji mikubwa;
- Kurahisisha utaratibu wa kumwona daktari bingwa ambao wanaonwa kwa ahadi maalum;
- Kuwapa fursa ya kujifunza na kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko kwenye hospitali za mikoa hiyo.
4.0 MAFANIKIO YA MPANGO HUO:
Mpango wa kupeleka Madaktari Bingwa mikoani umekuwa na mafanikio makubwa kwa maana ya kuwafikia walengwa ambao wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari hao. Maisha ya watanzania yameokolewa kwa huduma zitolewazo na Madaktari Bingwa unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mikoa ya Lindi, kigoma, Katavi na Rukwa imeshafikiwa na mpango huo na idadi ya wananchi waliopata huduma hiyo ya madakatari bingwa ni kama ifuatavyo:-
SN | MKOA | WAGONJWA WALIOONWA | WALIOFANYIWA OPERESHENI |
1 | Lindi | 258 | 6 |
2 | Kigoma | 754 | 37 |
3 | Katavi | 1276 | 37 |
4 | Rukwa | 1410 | 18 |
Jumla | 3,698 | 98 |
Mpango huu umepokelewa kwa mtizamo chanya na wadau wetu wakiwemo wanachama na wananchi wa mikoa husika kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo nyingi ziko mbali na maeneo wanayoishi.
5.0 RATIBA YA MIKOA INAYOFUATA
Mikoa inayofuatiwa kupelekewa huduma hii ya madaktari bingwa ni Mara,Tabora, Manyara na Mtwara.
5.0 RATIBA YA MIKOA INAYOFUATA
Mikoa inayofuatiwa kupelekewa huduma hii ya madaktari bingwa ni Mara,Tabora, Manyara na Mtwara.
MKOA | TAREHE | MAHALI HUDUMA ZITAKAPOTOLEWA |
Mara | 3/11/2014-8/11/2014 | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara |
Tabora | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Manyara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Mtwara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) |
CHANGAMOTO ZA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI:
Pamoja na nia njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka madaktari Bingwa karibu zaidi ya wananchi wengi wenye mahitaji ya huduma zao, bado zoezi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo:
- Idadi ndogo ya Madaktari Bingwa ikilinganishwa na wananchi wanaohitaji huduma hizo.
- Uhaba wa vifaa tiba vya kisasa, kama vile vipimo katika hospitali za mikoa ya pembezoni na
- Uhaba wa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha zoezi hili.
- Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaamini kuwa mpango huu utaokoa maisha ya Watanzania wengi ambao walikwishakata tamaa ya kupata tiba kutokana na gharama kubwa za kufuata matibabu hayo katika hospitali walizopewa rufaa.
6.0 MIPANGO YA BAADAYE YA MFUKO.
Mfuko utaendelea kupeleka Madaktari Bingwa katika maeneo mbalimbali ya nchi baada ya kufanya upembuzi wa mahitaji ya huduma na utaalamu katika maeneo husika.
Kauli mbiu yetu ni “ Afya Bora Ndiyo Mambo Yote.”
No comments:
Post a Comment