THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana, kufuatia kifo cha Capt. Mstaafu John Rwezaura Barongo kilichotokea tarehe 20 Octoba, 2014 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
“Chama kimempoteza mtumishi wake wa muda mrefu na muaminifu, ambaye amefanya kazi zake bila kuchoka na hata baada ya kustaafu amebakia kuwa muaminifu na mwanachama imara”. Rais amesema na kuongeza kuwa Marehemu amekuwa mtumishi hodari katika Jeshi, Chama na Serikali , hivyo mchango wake utathaminiwa siku zote.
Kupitia kwa Katibu Mkuu wa CCM, amewatumia salamu familia ya marehemu, wana CCM, ndugu na jamaa wote ambao wamekuwa karibu na marehemu.
Marehemu Capt. Mstaafu Barongo alizaliwa Disemba 1, 1942 katika kijiji cha KatojaWilaya ya Bukoba Mjini Mkoani Kagera.
Alianza utumishi wake katika Chama cha TANU Mwaka 1963 na kuendelea hadi CCM katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Manyara, Shinyanga, Dar es Salaam na Dodoma.
Marehemu ameacha Mke na watoto kadhaa.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba, 2014.

No comments:
Post a Comment