Baadhi ya Wanasalamu wa kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu njiro jijini Arusha wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa uongozi wa hospitali ya mkoa Mt.meru jana,kulia ni mratibu wa salamu kupitia kipindi cha usiku wa moto Yacob Simba kushoto ni Sista Shubi Mjawizi,anayefatia ni Sista Merry Stalla
Yacob Simba akiongea na baadhi ya wanasalamu katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru anayefatia ni Godfrey Thomas ambao ni waratibu wa shughuli hiyo kupitia kituo cha Redio 5 katika kipindi usiku wa moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima
Yacob Simba akikabidhi ndoo ya mafuta kwa uongozi wa hospitali ya Mt.Meru jana baadaa ya wanasalamu kutoka mikoa zaidi 21 kufika hospitalini hapo kuwafariji wagonjwa
Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha,katikati ni Yacob Simba na Godfrey Thomas wakiwa wanajadili jambo
Kulia ni Lucy Bongole ambaye ni mwanasalamu wakiwa wanajadiliana na wenzake katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru katikati ni Zuhura Mbise maarufu kwa jina la mama Sosy,kushoto ni Sister Monduly
Kushoto Mtangazaji maarufu wa Redio 5 kupitia kipindi chake cha love cuts kinachorushwa jumatatu hadi ijumaa saa nne hadi saa saba usiku Semio Sonyo akiwa na mtangazaji machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha usiku wa Moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima Godfrey Thomas aka GT wakifurahia jambo
Nesi wa hospitali ya Mt.Meru Sista Merry Stella akitoa neno la shukrani kwa wanasalamu waliofika kuwatembela wagonjwa hospitalini hapo ambapo amewataka watu na mashirika mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwa mahitaji ya wagonjwa ni makubwa
Wapili kulia ni mmiliki wa jamiiblog Pamela Mollel wakwanza kushoto ni Godfrey Thomas aka GT wakiwa katika picha na baadhi ya wanasalamu jana zoezi hilo liliratibiwa na kituo cha Redio 5 kupitia kipindi cha usiku wa moto
Baadhi ya wanasalamu wakisubiria kuingia katika wodi mbalimbali kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo
"Pole mama Mungu atakuponya"hayo ni maneno ya wanasalamu
Mwanasalamu mkongwe kutoka Arusha Baba Ali Mbondei(aliyevalia tisheti ya Redio 5)akiwa na wanasalamu wenzake wakimjulia hali mgonjwa katika wodi ya wanaume
Wanasalamu wakiwa wanasoma dua kwa mgonjwa wodi ya wanaume katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
Godfrey Thomas aka GT katikati akiwa amepozi na mashabiki wake ambao ni wanasalamu kupitia kipindi cha usiku wa moto cha kituo cha Redio 5 jijini Arusha
Wanasalamu kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa (Habari Picha na Pamela wa Jamiiblog)
No comments:
Post a Comment