Mtaa wa Garden ulioko jijini Dar es Salaam umebadilishwa jina na kuwa Hamburg Avenue.
Hafla ya kubadili jina hilo ilifanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, amesema uamuzi wa kubadili jina la mtaa huo limetokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania na jiji la Hamburg la nchini Ujerumani .
Kutokana na ushirikiano katika majiji hayo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kikosi cha zimamoto, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Philip Mwakyusa amesema Serikali ya Ujerumani itasaidia katika ujenzi wa mtambo wa kutengeneza mbolea kwa kutumia taka ngumu.
No comments:
Post a Comment