Kuishi maisha halisi yenye furaha na maana kwako ni kitu cha thamani sana. Unayo kila sababu ya kufuata njia yako ya maisha yenye misingi mizuri ya kukujenga katika kila nyanja ya maisha yako. Kwa kuwa kila mtu ana maono yake binafsi kuhusu maisha ni vigumu kufafanua maana halisi ya maisha. Naamini nawe pia una falsafa yako ya kutafsiri nini maana ya maisha mazuri kwako, ushauri huu hapo chini utakusaidia kufafanua vizuri zaidi maana halisi ya maisha yako.
1. Kuwa mkweli kwako mwenyewe.
-Maisha mazuri hutafsirika na mtu mwenyewe, labda mimi naweza kukuambia maisha mazuri kwangu ni kuwa mwenye furaha na familia yangu, afya njema, kijana mtanashati, hodari na mwenye kujitegemea mwenyewe. Nawe pia una maono yako labda ni tofauti na yangu, ni hayo maono yako ndiyo yanayokutambulisha na kukufanya uishi kwa misingi uliyojiwekea. Faraja katika maisha yako hupatikana pale unapopata ulichokuwa ukikitamani kwa muda mrefu. Lakini pia faraja hii huletwa na kuongezeka zaidi pale wewe mwenyewe kutoka moyoni mwako unapoamua kufurahi kwa kile kidogo au kikubwa ulichonacho.
2. Tathmini mabadiliko yako binafsi katika nyanja mbalimbali za maisha yako.
-Hakuna mtu aliyekamilika, kila mtu ana kila sababu za kukua kimaadili, kiimani, kielimu, kimahusiano na watu wanaomzunguka nakadhalika. Maisha ni kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda mahali pengine palipo bora zaidi. Mabadiliko haya ya kimaendeleo huongeza utu wa mtu hivyo huongeza faraja na kuleta maana nzuri ya kubadilika kwako katika jamii na kuwa mfano wa kuigwa.
-Hakuna mtu aliyekamilika, kila mtu ana kila sababu za kukua kimaadili, kiimani, kielimu, kimahusiano na watu wanaomzunguka nakadhalika. Maisha ni kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda mahali pengine palipo bora zaidi. Mabadiliko haya ya kimaendeleo huongeza utu wa mtu hivyo huongeza faraja na kuleta maana nzuri ya kubadilika kwako katika jamii na kuwa mfano wa kuigwa.
3. Jikubali mwenyewe bila kujali mapungufu yako au kasoro ulizonazo.
-Mapungufu na kasoro ulizonazo ndizo zinazokufanya wewe uonekana ulivyo sasa. Kujifariji ni namna ya kujitambua na kujielewa vizuri kwasababu ukijipenda na kujikubali mwenyewe ni rahisi kwako kuwapenda na kuwakubali watu wengine. Kujielewa ni mwanzo wa kuishi vizuri kwakuwa hutokubali hasira, jaziba au majonzi ya aina yoyote ile yakutawale na kuwa huru mwenye furaha na maisha yako. Watu wa aina hii wanaoishi kwa kujielewa huelewa pia mazingira yao hivyo ni wepesi kusamehe na kutatua matatizo yao kwa njia iliyo sahihi bila stress au ku-panic wanapopatwa na tatizo
Kujua namna ya kumudu stress download hichi kitabu: Download this Managing Stress ebook for Free.
4. Ishi maisha ya kutaka maendeleo endelevu.
-Maisha ni safari ndefu, ungependa kuishi maisha ya namna gani? Jibu unalo mwenyewe kwakuwa wewe ndiye mwenye maamuzi ya kujua nini unataka. Safari ya maisha hutafsirika vizuri kutokana na mafanikio na makosa ya mtu aliyopitia.
Safari hii ni ya kujifunza, kujirekebisha na kukua imara zaidi. Safari yenyewe huusisha yale tuliyoshinda na yale tuliyopoteza pia. Kujifunza kunahusu kufanya makosa na kujisamehe kwa yale tuliyokosea. Kwa kujifunza makosa hayo tunatakiwa kusonga mbele na kuyaendea malengo tuliyojiwekea.
Kujua zaidi: Soma Mbinu za kukusogeza karibu na malengo yako.
5. Ishi kila siku kulingana na mambo unayoamini yana misingi mizuri kwa maisha yako.
-Hakuna anayejua nini kitatokea kesho isipokuwa tuna imani na yale tuliyopanga yatakwenda vizuri kama tunavyotaka yawe. Huwezi sema sina furaha leo kwasababu sina kitu fulani au mpaka jambo fulani litimie. Ukifanya hivyo utakuwa unakosea kwani maisha ndio sasa na sio baaadae. Kila wakati jiweke safi na jisikie furaha kama unavyotaka, jione wewe ni kama kioo ya kile unachotamani kutimiza katika ndoto zako na kwa kufanya hivyo utakuwa mwenye furaha na maisha yako huku ukiendelea kujibidiisha na kufuata ndoto zako ulizojiwekea kwa kuwa mvumilivu na ipo siku ndoto zako zitatimia na kuwa kweli.
6. Kuwa mjanja kuona fursa za pekee kila zinapotokea katika maisha yako.
-Wakati mwingine fursa zinakuja kimya kimya pasipo kubisha hodi. Kuwa makini ili uweze kuzitambua kwani si kila kitu utaambiwa hichi au kile kina manufaa kwako. Jiwekee malengo ili fursa sahihi inapokuja ujue nini cha kufanya.
7. Tambua wakati wowote unayonafasi ya kufanya maamuzi ya maisha yako.
-Katika hali yoyote ile ya maisha yako ni wewe ndiye mwenye jukumu la kuamua nini unataka. Kama unaona kitu fulani hakipo sawa katika maisha yako basi kibadilishe. Mambo yako yatarekebishwa na kuwa vizuri na wewe mwenyewe. Hakuna kitu kizuri kinachoweza kufanyika isipokuwa kwa kufanywa na wewe mwenyewe.
BY LIFE SKILLS
No comments:
Post a Comment