Mtoto Baraka Deogratias mwenye umri wa miaka tisa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kitunda jijini Dar es Salaam,amedaiwa kuuawa na baba yake wa kambo baada ya kumpiga kwa kosa la kutosahishiwa baadhi ya madaftari yake ya shule na kusababisha mtoto huyo kupoteza maisha.
Mama mzazi wa marehemu Baraka Bi Veronica Jeremiah amesema siku ya Jumamosi ya tarehe 5 Octoba 2013 saa 2 usiku mume wake bwana Masaka Limbu alifika nyumbani na kuanza kukagua madaftari ya watoto wawili ambao ni Pita masaka ambaye ni mtoto halali wa mtuhumiwa na Baraka Deogratias ambaye ni mtoto wa kambo wakiwa chumbani na baba yao alisikia kilio cha mtoto wake ambaye ambaye hakuzaliwa na mume huyo akilia kwa uchungu lakini alipofika alikuta hajiwezi na alipomkimbiza katika zahanati ya eneo hilo,mtoto alipoteza maisha huku baba halali wa marehemu akionyesha kuumizwa na kifo cha mtoto wake.
Baadhi ya wazee wa eneo hilo wamemlalamikia mtuhumiwa bwana Masaka Limbu,kwa tabia yake ya kupenda ugomvi na kuongeza kuwa kuna adhabu zingine zinazidi mipaka katika kumwadhibu mtoto huku mtoto mdogo aliyeshuhudia hali hiyo akisimulia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi ilala Acp Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku mkurugenzi mtendaji wa tamwa Bi Valerie Msoka akieleza akionya jamii kuachana na vitendo vya ukatili ndani ya jamii ambavyo vinasababisha madhara makubwa na kugeuka kuwa majuto katika maisha yao.
Mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam wakati familia ikisubiri jeshi la polisi kutoa idhini ya mwili huo lini izikwe.
No comments:
Post a Comment