TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Thursday, 10 October 2013

WADAU WA UTEPE MWEUPE WA UZAZI SALAMA TANZANIA WAFANYA MKUTANO MKOANI RUKWA

 
Mratibu wa taifa wa utepe mweupe wa Uzazi salama Tanzania Mama Rose Mlay akizungumza katika Mkutano wa siku moja kati ya Uongozi wa Mkoa wa Rukwa, viongozi wa dini, wabunge, viongozi wa asasi za kijamii na za kidini na Muungano wa utepe mweupe wa Uzazi wa Salama Tanzania katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe 8 Oktoba 2013. Akielezea malengo ya mkutano huo alisema Serikali ya Tanzania inaheshimu ahadi yake ya kuwa na asilimia hamsini ya vituo vya afya Mkoani Rukwa vitakavyotoa huduma kamili za dharura za uzazi zikiwa ni pamoja na upasuaji kumtoa mtoto na kutoa damu salama zinapohitajika ifikapo 2015. Ktikati ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla.
Vikundi kazi katika kujadili mpango mkakati utakaotumiwa kuendeleza umuhimu wa huduma za uzazi salama katika jamii.
Dkt. Lunyelele akichangia moja ya mada katika Mkutano huo.

Picha ya pamoja
Chakula cha pamoja. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
 
 

No comments:

Post a Comment