TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday 5 October 2013

AJALI MBAYA JIJINI DAR ES SALAAM TAKRIBANI WANAFUNZI 50 WANUSURIKA


 Askari wa usalama barabarani wakijipanga kutoa huduma baada ya basi la daladala lililokuwa limebeba wanafunzi takriban 50 wa shule ya msingi ya Mgulani kugongana na gari dogo aina ya RAV 4 na kupinduka katika makutano ya Kenyatta Avenue na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam leo jioni. Dereva wa gari dogo akiwa na mtoto wa umri wa takriban miaka mitatu walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali. Wanafunzi wote walinusurika. Haijafahamika ni nini chanzo cha ajali hiyo ambayo basi lilikuwa likitokea kaskazini wakati gari dogo lilikuwa likitokea kusini.
 Uharibifu wa miundumbinu baada ya ajali hiyo
 Askari wa usalama barabarani wakiondoa mabegi ya wanafunzi hao ambao walitafutiwa basi lingine kuwapeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi
 Wanafunzi wakiwa katika gari walilotafutiwa baada ya ajali hiyo
 Magari ya break-down yakifanya juhudi ya kunyanyua basi hilo
Baadhi ya wanafunzi hao baada ya ajali. Ishukuriwe hakuna aliyeumia
 
POWERED BY MICHUZI


 

No comments:

Post a Comment