TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Sunday, 27 October 2013

SIKU 71 ZATOLEWA KWA VINARA WA UNGA WASALIMU KWA RAIS KIKWETE AU WABRUTWE ICC.

 

Viongozi wa dini wametaja majina 61 ya vinara wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini ambao wanatarajia kuwaburuza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kujibu tuhuma zao. Majina hayo yametajwa na Kamati ya Maadili na Haki za Jamii kwa Viongozi wa Dini na Wananchi nchini, ambapo miongoni mwao wamo wabunge wa majimbo na viti maalum, mawaziri, viongozi wa dini na wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipendekoste, William Mwamalanga, aliliambia gazeti hili

(NIPASHE) kuwa, majina hayo yalipatikana Jumanne wiki hii kupitia mkutano wa siri wa viongozi wa dini wa madhehebu ya kiislam na kikristo 134 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Pemba.

Mkutano huo ambao ulifanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 21, mwaka huu hapa jijini Dar es Salaam uliwakilishwa na viongozi wawili wa dini kila mkoa isipokuwa Rukwa ambapo hapakuwa na mwakilishi. Alisema ulifanyika kwa siri ili kutotoa mwanya wa kuingiliwa na mifumo isiyo rasmi ambayo ingevuruga adhima yao.

Kuhusu upatikanaji wa majina, mchungaji huyo alisema ulitokana na utafiti walioufanya ndani na nje ya nchi. Pia alisema taarifa nyingine walizipata kupitia kwa wasiri wao kutoka ndani ya jeshi la polisi nchini na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka nje ya nchi.

Akizungumzia mkutano huo, alisema lengo lake lilikuwa ni kutathmini biashara za dawa hizo ambazo alieleza ni tishio linaloangamiza kwa kasi kubwa vijana na kusababisha nchi kuingia kwenye aibu duniani. Mchungaji Mwamalanga alisema katika mkutano huo walitoka na maazimio mawili likiwamo la kuwafikisha mahakamani wahusika na kufanya kampeni za siri kupita kwenye majimbo sita ya wabunge (majina tunayo) waliotajwa. Alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwaeleza wananchi tabia za wawakilishi wao ili mwaka 2015 waweze kuchagua viongozi bora wenye uchungu na nchi yao, wakereketwa wa amani na watakaochochea watu kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Alisema wakati wa uchaguzi mkuu wawakilishi wa mkutano huo, watapita tena majimboni kuwataja wahusika kwa majina.

Kuhusu viongozi wa dini ambao wametajwa kujihusisha na biashara hiyo, mwenyekiti huyo alisema, mkutano umewataka wafuate mfano wa Mchungaji Donald Mwakisambwe wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste nchini, aliyeacha kwa ridhaa yake.

Aidha, kamati hiyo imetoa siku 71 kuanzia Jumanne ya wiki hii kwa wahusika wote 61 kujisalimisha wenyewe kwa Rais Jakaya Kikwete: “Wakati mchakato wa kuyapeleka majina haya ICC ukiendelea tunawataka wahusika wajisalimishe kwa Kikwete kwa kuwa orodha hii tuliyonayo (akitaja majina yao) ni miongoni mwa wale waliotajwa kwenye orodha aliyokabidhiwa Rais wakati ule, wakijisalimisha tutajua kupitia wasiri wetu,” alisema na kuongeza: “Vinara hawa ambao Watanzania wamekuwa wakiwaita ‘vigogo wa dawa za kulevya’ hawapaswi kuitwa jina hili, hawa ni wahuni na wauaji, tusiwape majina mazuri ambayo yanawatukuza ndiyo maana biashara hii inakuwa kwa kasi,” alisema.

Kuhusu Watanzania 175 waliokamatwa nchini China ambao wanasubiri adhabu ya kunyongwa na wengine waliowahi kukamatwa nchi nyingine duniani alisema, utafiti waliofanya unaonyesha kuwa wengi wao hutumwa na wakubwa hapa nchini na kuahidiwa fedha nyingi: “Tumekubaliana wakati vijana wetu wakisubiri adhabu hiyo ya kunyongwa basi ICC iwatambue wahuni (vigogo) wanaosababisha biashara hii hapa Tanzania,” alisema.

Alisema katika mkutano huo wa siri alikuwapo mtaalam wa sheria mstaafu aliyekuwa akifanya kazi katika mahakama ya ICC ambaye amewasaidia jinsi ya kufungua kesi hiyo mahakamani hapo.

Malizia kusoma habari hii kwenye gazeti la
Nipashe

Huduma ya bure ya ushauri na tiba kwa wanafunzi na wazazi juu ya elimu, malezi n.k.

 

Picture

Adolescent Psychological Consultancy Services, nNi wataalamu waliobobea kwenye masuala ya 'psychological' na matatizo yake:

  1. Kwa vijana na wanafunzi wenye matatizo ya kusoma (learning difficulties)
  2. Hofu (anxiety) au woga wa kuongea kwenye hadhira au kufanya 'presentation'
  3. Elimu ya kupevuka (puberty education) kwa vijana wadogo
  4. Mbinu za kuwapa wazazi kwa ajili ya malezi (parenting skills orientation)

Puberty education, Learning difficulties therapy, Biopsychosocial/Screening/Assessment (Adults and Adolescents), Councelling (Individua and group), General health consultation,


Stress reduction, Referral services.

Mawasiliano/Our contacts:

Adolescent Psychological Consultancy Services (APCS),
P. O. Box 6469,
Haile Selassie Rd, Morogoro Store, OysterBay, 
Dar es Salaam,
Tanzania.

Mobile: 0713555729, 0754545586.
Email:i nfo@apcs.or.tz, mlengusi @yahoo.com
Website: www.apcs.or.tz
Facebook.com\apcstz
Twitter: @apcstanzania

Kwa sasa huduma hizi zinapatikana bure kwa ufadhili wa AMREF na SIDA kwenye kituo cha MYC Mwananyamala.

Njoo ukutane na madaktari wa akili na mwili, washauri wa elimu ya afya na mambo yahusuyo maisha kwa ujumla. BURE!

SHULE YA WAMA NAKAYAMA ILIYOPO RUFIJI YAFANYA MAHAFALI YA KWANZA

 
1Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipowasili katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari WAMA Nakayama yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani jana.Zaidi ya wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri akiwemo balozi wa Japan na wafanyabiashara ambapo mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi aliahidi kuisadia shule hiyo shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano.1aaRais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji. 2Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo. 4Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo 5Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shule hiyo Dr. Ramadhan Dau. 5aWahitimu wakiingia katika eneo la tukio 6Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi. 6bRais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania Mhe.Masaki Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwetena kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa. 7Baadhi wa walimu wa shule hiyo 7cBaadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu katibu mkuu taaisis ya WAMA na Dan Kiondo. 8Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama 8cMh. Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo

DUH!! WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, BALOZI ABRAHAM ISAAC SEPETU

Pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani, DR. William Nchimbi, akimpa pole Balozi Isaac Sepetu alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake September 21, 2013.
Wema (kulia) akiwa na baba yake (kati), kushoto ni meneja wake anayejulikana kwa jina la Petitman.
Balozi Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. PICHA: Maktaba/GPL

PAROKIA YA LUGOBA YAADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 100 RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NI MGENI RASIMI.

 n12 Rais Jakaya Kikwete  na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  wa Jimbo la Morogoro Onesphory  Mkude, wakishuhudiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Anthony Banzi,   wakiweka jiwe la msingi katika kiwanja kitakachojengwa jengo la vijana katika Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.n13Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  wa Jimbo la Morogoro Onesphory  Mkude, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Anthony Banzi, viongozi wa mkoa wa pwani na kamati ya walei ya Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 ya Parokia hiyo.m10Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  wa Jimbo la Morogoro Onesphory  Mkude, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Anthony Banzi, viongozi wa mkoa wa pwani na kwaya pamoja na watoto wa shule ya Jumapili katika  Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 Parokia hiyo.m6Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika  Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.i ya Miaka 100 wa Parokia hiyo. n2 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua zahanati katika Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.i ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.

n4Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Masista wa Parokia ya Lugoba n6Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi. n8Rais Jakaya Kikwete akiwaonyesha jambo  maaskofu wakati wa jumilee ya miaka 100 ya kanisa katoliki parokia ya Lugoba leo n10 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  wa Jimbo la Morogoro Onesphory  Mkude, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Anthony Banz na  viongozi wa mkoa wa pwani iliyokuwa inaendeshwa na darasa alilosomea wakati alipokuwa shule ya kati ilinayoendeshwa na Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo. PICHA NA IKULU 

Saturday, 26 October 2013

JENGO LA MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI NA HUDUMA ZA UPASUAJI WA MOYO MKOANI MWANZA,LAZINDULIWA RASIMI NA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akishuhudia zoezi la upasuaji wa Moyo alipokuwa akifanyiwa mmoja wa wagonjwa wa Moyo ndani ya Hospitali ya Bugando, baada ya kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza leo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo, katika Hospitali ya Bugando Mkoa wa Mwanza, wakati wa wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo
 Shughuli ya Upasuaji mgonjwa wa Moyo ikiendelea.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal (katikati) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika wakati wa upasuaji wa Moyo katika Hospitali ya Bugando
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando 'Bungado Day', iliyofanyika leo jijini Mwanza sambamba na uzinduzi wa Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia moja kati ya chupa ya mafuta ya Vaseline, ambayo ni 'Feki' yaliyokamatwa na TFDA, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo sambamba na uzinduzi wa Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa kati ya watoto 18 waliokwishafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Bugando kwa gharama ya SH. 50, 000/ badala ya gharama sahihi ya Sh. milioni 6. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, leo amehudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo na kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza.Picha na OMR

PATA YALIYOJIRI HUKO KILINDI,TANGA

Idadi kubwa ya askari polisi FFU imepelekwa wilayani kilindi ili kuongeza nguvu kwa askali wenzao ambao inaonekana kuzidiwa nguvu na kundi lililofanya vurugu iliyosababisha kujeruhiwa kwa risasi OCD wa Kilindi.

Kundi hilo liliwasili hapa handeni majira ya saa 5 usiku, likitokea kibaha pwani, na lilikua linaongozwa na mkuu wa wilaya ya kibaha. Msafara huo ulipita kuonana na mkuu wa wilaya ya handeni ili kupata maelekezo toka kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa tanga, ambao walikutana hapa handeni kujadili hali tete ya handeni.

Kikao hicho kilidumu takribani masaa 5 tangia saa 9 hadi 1 ucku. Kikao hicho kilifanyika HILL TOWN HOTEL.
Picture
Askari majeruhi (picha kutoka kwa Assenga Oscar)

Endelea kusoma hapo chini, taarifa kama zilivyoripotiwa na watu mbalimbali kuhusu suala hili: