Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)
tangaza hapa
TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA
Thursday, 2 October 2014
UMOJA WA VYUO VYA USAFIRI WA ANGA BARANI AFRIKA(AATO)TANZANIA YAWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA KWANZA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)
ORIFLAME YATOA AJIRA 60,000,PIA YAZINDUA BIDHAA MPYA JANA TAREHE 01 OCT2014
Mkurugenzi Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Japhet Naftal (kulia), akifungua mkutno kwa makofi maalumu ya Oriflame katika hafla hiyo ya kutangaza bidhaa mpya za Kampuni hiyo iliyofanyika katika ofisi zao Dar es Salaam jana jioni zilizopo Posta Mpya ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor..
Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya (kulia), akizungumza na wanachama wa kampuni hiyo kuhusu bidhaa mpya na mipango ya miezi mitatu ya kampuni hiyo. Moja ya bidhaa mpya iliyonadiwa na kutangazwa ni The One Make -Up sanjari na kuzindua kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia jana Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.
Viongozi wa Kampuni hiyo wakitambulishwa kwa wanachama. Kutoka kushoto ni Jesca Nisege, Meshack Wayanje, Julieth Msofe, Clara Wekwe, Christina Basil, James Mwangamba na Nasra Mohamed.
Wanachama wa Oriflame Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja Mkazi, Fortunata Nkya wakati akielezea mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.
Warembo wa Oriflame wakiwa katika sura ng'avu baada ya kutumia vipodozi vinavyosambazwa na kampuni hiyo hakika wanapendeza, wakina mama nunueni vipodozi vya Oriflame ili mpendeze kama akina dada hawa. Kutoka kushoto ni mrembo Monica Mhando, Zainabu Ali na Suhaila Abdallah.
Ofisa Mwandamizi wa Oriflame Tanzania, James Mwangamba akihojiwa na wanahabari hapo anaelezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kampuni hiyo.
KAMPUNI ya Oriflame Tanzania inayouza vipodozi asilia imetoa ajira kwa vijana 60,000 wa kitanzania kwa kusambaza na kuuza bidhaa zake.Hayo yalibainishwa na Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana katika hafla ya kutangaza bidhaa mpya na uzinduzi wa kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.
"Tangu tuanzishe kampuni hii mwaka 2011 tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 60,000 jambo ambalo tunajivunia ukizingatia changamoto kubwa ya uhaba wa ajira" alisema Nkya.Alisema vijana hao wamekuwa wakijipatia zaidi ya sh. milioni 10 kwa mwezi kutokana na kufanya biashara ya bidhaa zetu kwa mfumo wa moja kwa moja.Nkya alisema kampuni yenye makao yake makuu nchini Sweden kila baada ya miezi mitatu inaingiza bidhaa mpya sokoni ili kutoa fursa kwa wateja wao kuzipata kwa urahisi na kuzisambaza kila kona kupitia mtandao wa vijana waliopo katika makundi.Aliongeza kuwa bidhaa nyingi ni vipodozi asilia vinavyotumika kwa wanaume na vingi zaidi ni kwa ajili ya wanawake.Nkya alitumia nadfasi hiyo kuwahamasisha wanawake kote nchini kununua vipodozi kutoka Oriflame Tanzania kwani havina kemikali yoyote ni bora na salama kwa mtumiaji kwa wakati wote.
Meneja huyo mkazi alisema kama atahijai ufafanuzi kuhusu namna ya kuzipata bidhaa zao anaweza kufika katika ofisi ya Oriflame iliyopo ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor.Imeandaliwa na mtandao wa (www.nkema.blogspot.com) na Getrude Edwrd.
x
Friday, 21 February 2014
PATA NAKALA YAKO PIGA NO.0784670746
Kutana na producer chipkizi Hilda Ngaja, kwenye movie iitwayo ( He Hurts me ) ambayo iko sokoni tayari. Pata nakala yako bila kukosa, pia unaweza letewa ulipo kwa kupiga no 0784670746 au wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa facebook www.nkema.blogspot.com.
post by
Nkema
Sunday, 9 February 2014
WASOME HAPA WAJUMBE WABUNGE MAALUM LA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Thursday, 23 January 2014
JINSI YA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KWA NJIA BORA ZAIDI
Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.
NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA
Ukitaka kufanya biashara yoyote ile unatakiwa kufanya utafiti. Kutokufanya utafiti ni chanzo cha biashara nyingi kuharibika. Lazima ujiulize kwamba unataka kufanya biashara gani? Usiseme unataka kufanya biashara yoyote ile kwani kusema kwamba unataka kufanya biashara yoyote ile ni kupoteza mwelekeo kwa kuwa utakuwa hujui unataka kufanya nini. Kama hujui cha kufanya hakuna kitu utakachokifanya. Hili ni tatizo la watu wengi. Hata baadhi ya watu niliokutana nao wakitaka ushauri wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili. Njia ya kukusaidia kuamua ufanye biashara gani ni kwa kujiuliza umewahi kufanya kazi au biashara gani? Umesomea nini? Vipaji vyako ni vipi? Ni biashara ipi au kazi ipi unapenda zaidi kuliko nyingine na kwa sababu gani? Ukisha jiuliza maswali haya chukua kalamu na karatasi uandike maswali yako na kuyajibu. Ukikagua maswali na majibu yako utagundua shughuli unayoipenda, unayoiweza na una kipaji nayo na hiyo ndiyo inayokufaa. Ukishachagua biashara unayoipenda ni rahisi sana kufanikiwa kwani shughuli utazifanya kwa hiyari bila kujilazimisha. Kama unashindwa kuamua ni biashara gani ufanye, soma sura ya sita katika kitabu hiki. Nimeelezea kuhusu mawazo yanayoweza kukusaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya. Kama utakuwa bado hujafikia uamuzi baada ya hapo basi tafuta na wasiliana na washauri ili mbadilishane mawazo na ufundishwe jinsi ya kuamua ufanye biashara gani.
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
Sunday, 5 January 2014
WANAWAKE WA SHOKA ULIMWENGUNI AKIWEMO MAMA GETRUDE MONGELA. SOMA HISTORIA YAKE FUPI
Kama kuna wanawake wa kitanzania ambao wameweza kuionyesha dunia kwamba Tanzania nayo ina wanawake wa shoka, basi Mama Gertrude Mongella naye yumo tena katika namba ya juu, hakosi katika namba tatu bora za mwanzo...nani anabisha? Mama huyu ambaye ni mwanasiasa, mwalimu, mwanaharakati, mke na mama wa watoto wanne, ndiye yule aliyeuongoza mkutano wa nne wa dunia kuhusu wanawake uliofanyika Beijing China mwaka 1995. Na ni huyu huyu ambaye ni rais wa kwanza wa bunge la afrika lililoundwa mwaka 2004. Ndugu wasomaji wangu naomba mjue kwamba bunge hili si la kina mama peke yake, ni bunge mchanganyiko. Kwahiyo mwanamama huyu kitendo cha kuwabwaga wanaume wote wa Afrika tena katika uchaguzi wa mara ya kwanza si kitu masihara kabisa.
Kabla sijaendelea zaidi kuwapasha juu ya mambo ambayo mama huyu ameshawahi kuyafanya, ningependa niwadokeze kidogo juu ya maisha yake binafsi.
Mama Gertrude Mongella alizaliwa katika kisiwa cha Ukerewe, mkoani Mwanza mwaka 1945 akiwa ni mmoja kati ya watoto wanne katika familia yao. Baba yake Patrice Magologozi alikuwa ni mjenzi, fundi seremala na mwanaharakati akikabiliana na siasa za mkoloni. Mama yake Bibi Nambona alikuwa ni mkulima stadi. Alizaliwa kipindi ambacho ubaguzi kati ya watoto wa kike na wakiume katika jamii yao ulikuwa umeshika hatamu, wanawake walizuiliwa mambo mengi, mfano kuongea mbele ya wanaume, kula vyakula baadhi ya vyakula au sehemu zilizonona za nyama, mfano mapaja ya kuku,firigisi mayai na vinginevyo vingi. Gertrude aliliona hili na rohoni mwake hakukubaliana nalo kabisa, lakini anamshukuru sana baba yake ambaye alikuwa akimtia moyo na kumwambia asifungwe na hizo mila na desturi ale anachotaka, aseme anapoona pana ukweli na shule atakwenda.
Alipokuwa na umri wa miaka 12, alianza shule iliyokuwa ikiendeshwa na watawa wa Maryknoll Nuns, Shule hii ilikuwa na malengo ya kuwaelimisha na kuwanyanyua watoto wa kike. Na hii ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kusafiri toka azaliwe.
Baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata Shahada ya elimu. Mwaka 1975 aliingia katika siasa na kuwa mwanachama katika Baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki (EALA).
Tangu wakati huo, amekuwa akishikilia nafasi nyingi za uongozi katika Chama tawala na Serikali ya Tanzania, na nje ya nchi bonyeza hapa usome mwenyewe. Na kwa baadhi ya mahojiano ambayo amekwisha yafanya bonyeza hapa na hapa usome, na hapa umsikilize.
Watanzania hatuna budi kushukuru kuwa na mwanamke jasiri na muwezaji wa mambo kama huyu. Gertrude Mongella ni mtu asiye tishika na ndio sababu hata dunia imeweza kumuona. Na baada ya kumfuatilia sana nimegundua jambo moja, si mtu anayekurupushwa na matokeo ya jambo, ni mtu anayeangalia nini kiini au chanzo cha jambo hilo. Mfano ni pale alipozungumzia ya umaskini na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika bara la Afrika. Alisema kwamba" hebu tujiulize waafrika wengi wanaopigana utakuta wanamiliki silaha bora na za gharama mno, lakini mwafrika huyo huyo hana pesa hata ya kuweza kumnunulia mwanae kalamu!! Sasa hapo ujue lipo jambo.. ninani anayempa mwafrika huyu hizo silaha?? ..huyo ndiye wa kusakamwa kwani kama angekuwa na nia nzuri basi angempa kalamu au nyenzo za kufanyia kazi. Hebu usiache kumsikiliza katika kiungo nilichokuwekeeni hapo juu.
Zidumu fikra za Mama Mongella.
Subscribe to:
Posts (Atom)