Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa
habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4 za kurudufu CD feki
zilizokamatwa katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni
Ofisa wa Polisi, D/SSGT Daniel Gingo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa
========= ======= ======= =======
KAMPUNI
ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya
Mkurugenzi wake Alex Msama ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha
Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, imekamata
kompyuta za kufyatua kazi feki za wasanii zenye thamani ya mil18.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex
Msama, alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya
pande hizo tatu pamoja na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta,
mashine na kazi feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa
eneo la Kimara-Machungwani, jijini Dar es Salaam na mtuhumiwa huyo
amefikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya mchakato wa kiheria wa
kufikishwa mahakamani.
Msama
alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama
Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili,
amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi
ya wengine.Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo
cha mafanikio ya wahusika ambao licha ya kuifanya kazi hiyo kwa muda
mrefu, wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na wajanja hao
kuingiza kazi feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.
Msama
alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa
kushirikiana na wadau wengine, anashukuru kwamba kadiri siku
zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na ushirikiano ambao
wamekuwa wakipewa.“Msama Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza
Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa
kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,” alisema Msama.
Aliongeza,
kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga
mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi
katika kulinda maslahi ya wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo
ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata
vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo na kazi zenye jumla
ya shilingi bil.12.
Msama
alisema kampuni yake imejitwika jukumu hilo zito kwa lengo la kuona
wasanii wa Tanzania wananufaika na ubora wa kazi zao katika kuendesha
maisha yao kwamba kupitia vipaji vyao, wahusika waweze
kujiajiri.Alisema, katika mazingira ya sasa ambapo jasho la wasanii
linaishia mikononi mwa wajanja wachache ambao wamekuwa wakichakachua
kazi, kamwe wasani hawawezi kupata kipato cha kutosha kuboresha maisha
yao.
Msama
ametoa wito pia kwa wasamaria wema sio tu kutoa taarifa kwa kampuni
yake au Jeshi la Polisi za kuwafichua wanaojihusisha na uchakachuaji wa
kazi za wasanii, pia kuacha kununua kazi feki japo huuzwa kwa bei ya
kutupa.Baadhi ya wananchi walioshuhudia baadhi ya vifaa na kazi feki,
kwa nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi
hiyo ngumu kwa maslahi
ya wasanii.
Kelvin
Living na Iddy Abbas wa Mabibo, kwa nyakati tofauti, wameomba kazi hiyo
iwe endelevu kwa sababu wajanja hao wachache wanachangia wasanii kukosa
maslahi mazuri kupitia vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment