Fomu hizo za kutolea tamko zimeanza kutolewa na zinapatikana katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Dar es Salaam na katika ofisi za Kanda za Mashariki Kibaha, Arusha, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya taasisi kupitia www.ethicssecretariat.go.tz na katika tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz
Viongozi wa Umma wanapaswa kuelewa kuwa ni Ukiukaji wa Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Kiongozi kushindwa kurejesha Fomu za Tamko lake katika muda uliowekwa na Kiongozi atakayeshindwa kurejesha kwa tarehe husika atachukuliwa hatua kama ambavyo kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 kinavyoeleza.
Viongozi wa umma wanapaswa kukumbuka kuwa sio wajibu wa kisheria kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi kuwa pelekea viongozi fomu za tamko bali ni wajibu wa kiongozi husika kuzitafuta fomu hizo kwa wakati ili kutekeleza matakwa hayo ya kisheria.
IMETOLEWA NA
KAMISHNA WA MAADILI

No comments:
Post a Comment