TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 27 October 2014

Msichana asimulia ya Boko Haram

Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara
Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC.
Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo .
'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram.(P.T)
Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wanapinaji wa Boko Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana 200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale waliokimbia walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya watekaji.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewawateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua.

No comments:

Post a Comment