TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Wednesday, 22 October 2014

Allan Lucky aibukia kwenye "moja na mbili"

Allan Lucky
Allan Lucky

Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi maarufu cha Televisheni kinachohusiana na maisha ya wanafunzi wawapo shuleni, Allan Lucky a.k.a Rais wa Wanafunzi ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake nchini Kenya, ameibuka na kipaji kingine, U-Dj.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Allan Lucky amewaambia mashabiki wake kuwa kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi, atakuwa anatoa kupitia Hulkshare mixing mpya kali ambayo mtu yeyote anaweza kui-download na kuisikiliza mahali popote, iwe ni kwenye gari, nyumbani, house party na kadhalika. Unaweza kupitia ukurasa wake wa Hulkshare kupatamixing zote kali kutoka kwake hulkshare.com/AllanLucky

Mwezi huu ametoa mixing ya nyimbo za zamani za miondoko ya RnB ambazo zilipendwa sana miaka ya 90 na mwanzoni 2000. Unaweza pia kuipata kwa kuingia kwenye link hii:hulkshare.com/allanlucky/hotshit-mixx-11

Kwa taarifa zaidi,unaweza kutembelea kurasa zake za

Allan Lucky

No comments:

Post a Comment