Afisa mkuu msimamizi wa hospitali ya kijeshi ya Juba, Brigedia Gen Dr Ajak Bullen, ameambia shirika la redio la Miraya mjini Juba kuwa wanajeshi 66 wameuawa katika mapigano ya siku mbili.
Watafanyiwa mazishi ya pamoja.Wakati huohuo afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa watu 26 wameuawa katika mapigano ya siku mbili mjini Juba.Zaidi ya watu miamoja wamejeruhiwa huku maafisa wakuu wakijaribu kudhibiti mji huo kufuatia kile ambacho serikali ilisema ni jaribio la mapinduzi mbalo liliweza kutibuliwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin amesema kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wanajeshi watiifu kwa Riek Machar aliyekuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir anayedaiwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi.
Taarifa zinasema kuwa milio ya risasi ingali inasikika mjini Juba.
CHANZO NI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment