Wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakiwahoji matapeli (hawapo pichani) ambao walikua wakijaribu kumfanyia utapeli dada mmoja na hatimaye kushindwa kutimiza lengo lao mara baada ya dada huyo kushtukia mbinu zao na kuomba msaada kwa wananchi na ndipo hapo walipotiwa nguvuni na kupelekwa katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani
Matapeli (mwenye shati la draft) wakipewa kichapo mara baada ya kushindwa kujibu maswali ya wananchi waliowakamata leo katika kituo cha daladala cha Segerea
Mmoja wa watumishi wa serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya segerea Mfaume (wa kwanza kushoto Mwenye fulana ya njano) akijaribu kuwakata wananchi hao kujichukulia sheria Mikononi mara baada ya kuwatia nguvuni matapeli hao leo katika kituo cha daladala cha Tabata Segerea
Mmoja wa matapeli akijizuia kichwani mara baada ya wananchi wenye hasira kali wakiendelea kushusha kipigo kitakatifu, katika tukio la kujaribu utapeli lililotokea muda mfupi katika kituo cha daladala cha segerea mwisho
Hapa tapeli wa pili (aliyeinamishwa kichwa) akiendelea kupokea maumivu kutoka kwa wakazi wa segerea mara baada ya kukamatwa wakati wakitaka kujaribu kutapeli
kipigo kikiendelea kutolewa kwa matapeli hao
Matapeli wakiwa ndani ya ofisi ya serikali ya mtaa wa migombani mara baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi muda mfupi uliopita katika kituo cha daladala cha segerea mwisho wakati wakijaribu kutapeli
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakichungulia dirishani katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani kwaajili ya kushuhudia matapeli waliopokea kichapo cha mbwa mwizi mara baada ya mbinu zao kufua dafu na kushtukiwa
No comments:
Post a Comment