TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday 19 October 2013

MUUAJI WA MAMA YAKE FOO SARO AZIKWA BILA IBAADA YA KANISA


Marehemu Anthery Mushi Azikwa Uru, Kilimanjaro.
Kilimanjaro, Tanzania. Anthery Mushi aliyejiua Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya kujipiga risasi amezikwa kijijini kwao, Omgoma eneo la Uru mkoani Kilimanjaro bila kupatiwa huduma za kanisa kabla ya kuzikwa


Kabla ya kujipiga risasi, Mushi alimua mkwe wake, Anastazia Saro baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi kwa risasi aliyekuwa mzazi mwenzake, Ufoo Saro ambaye ni mwandishi na mtangazaji wa ITV na Radio One.

Licha ya Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru kushindwa kutoa huduma kwa marehemu kutokana na kujiua, ndugu wa marehemu walimuangukia Paroko wa Parokia ya kanisa hilo ili asome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.

Mbali na hayo, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi amesema Watanzania hawapaswi kumshutumu kijana huyo kwa hatua aliyoichukua kwani sasa imetosha kumshutumu. 

"Kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya kutokea kwa tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo," amesema baba mdogo wa marehemu huyo.

Ufoo Saro sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

No comments:

Post a Comment