TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Sunday, 6 October 2013

DIAMOND NAE AANZA KUJITABILIA!! SIKILIZA WIMBO HUU


Mwanamziki namba 1 kwa kupiga show hapa Tanzania Diamond Platnumz hivi karibuni alitoa maneno akizungumza siku akifa itakuwawaje kitu ambacho kilizua maswali mengi sana kwa mashabiki wake ambao hawakutegemea hata siku moja kama atakuja kusema maneno kama hayo kwa mashabiki wake kwani yalizua mining'ono mingi sana. Katika kusema hayo maneno Diamond alisema ni moja kati ya nyimbo ambayo ameiandika na inamtoa machozi kia aisikapo.

Baadhi ya mashairi katika nyimbo hiyo alisema:

Vipi Maneke atanililia...??
Je wasanii wenzangu wataniimbia..??
Ama litafutika jina langu...??
Na nyimbo zangu hawatasikia..??
Vipi wasafi watanililia....??
Je ndugu rafiki watahudhuria..?? 
Ama nitakapokufa Sina changu..??
Hata mama yangu watamkimbia...??


Kwa mara ya kwanza pata kuisikiliza na kudownload nyimbo hiyo yenye maneno ya kuudhunisha kutoka kwa Diamond

No comments:

Post a Comment