TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday, 21 December 2013

TAZAMA VITUKO VYA RIHANNA

http://theclicktz.com/

http://theclicktz.com/

http://theclicktz.com/
Msanii mkali wa pop, huko marekani Rihanna amekuwa akisikika sana kwa vituko vyake, hivi karibuni alionekana akiwa amevaa Nusu uchi huku akikatika, wakati alipoenda kutembelea kwao, nakufanya shuhuli za kimila. Imekuwa ni kawaida kwa kuvaa nusu uchi na kupita mitaani au hata kwenye maenyesho yake

ATIWA MBARONI KWA KUOA WANAFUNZI, MTU NA DADAYE.


                            OFISA USITAWI WA JAMII WA HALIMASHAURI WA WILAYA YA MKASI,OSCAR MDENYE

JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi.

Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano (umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni dada wa binti wa pili.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema walimfuatilia Jacob na  
kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao.

“…Tulikuwa katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye kumkamata mtuhumiwa,” alisema Kisimba.

Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10, 2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16) aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume.

Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho, kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na kuanza kuishi naye.

“…Hadi Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12) kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na kulazimishwa kuolewa,” alisema Mdenye.

Juhudi za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili.

Hata hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka, kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi 143 zimeripotiwa wilayani hapo.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA

ZITO KABWE ATUA MKOANI KIGOMA KWA KISHINDO, APOKEWA NA MAANDAMANO MAKUBWA. SOMA HOTUBA YAKE


  Sehemu ya Vijana wakiandaman kwa furaha muda mfupi baada ya kumpokea mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuwasili kigoma leo
 
 Baaadhi ya Madreva bodaboda mkoani kigoma wakiongoza msafara wa mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema Zitto Kabwe muda mfupu baada ya kuwasili
  Sehemu ya Vijana wakiandaman kwa furaha muda mfupi baada ya kumpokea mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuwasili kigoma leo
 Mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema Zitto Kabwe(wa tatu kulia)akilakiwa na baadhi ya viongozi wa chadema mkoani Kigoma muda mfupu baada ya kuwasili na kupokewa na maandamano makubwa
 Mbunge wa kigoma kaskazini-Chadema  akisalimiana na mamiaaaaa ya wanakigoma muda mfupi baada ya kuwasili na kupokelewa na maandamano makubwa mjini kigoma leo
Mbunge wa kigoma kaskazini -chadema Zitto Kabwe Akihutubia maelefu ya wananchama na wapenzi wa chadema muda mfupi baada ya kuwasili mkoni kigoma leo na kupokelewa kwa maandamano makubwa.

Thursday, 19 December 2013

MBEYA:Mamlaka ya udhibiti wa chakula,dawa na vipodozi(TFDA) kanda ya nyanda za juu kusini imezifunga machinjio mbili Mkoani humo.



Hii ni machinjio ya Mbalizi iliyofungwa



Kaimu Meneja wa Kanda nyanda za juu Kusini,Rodney Alananga, alithibitisha kufungiwa kwa machinjio hizo na kwamba sababu za kufunga machinjio ya Uyole Jijini Mbeya ni kutokana na  kutokuwa na miundo mbinu mizuri ya maji hivyo kuhatarisha afya za walaji na wakazi walio kando ya machinjio.

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Magreth Akilimali, alilazimika kutembelea na kujionea hali halisi ya uchafu uliokithiri na kuahidi kuwa watafanya usafi eneo hilo kwa muda wa siku tano kuanzia Desemba 14 kwa kutumia gari la kunyonya maji machafu la Halmashauri ya Jiji la Mbeya.







MAMLAKA ya udhibiti wa chakula,dawa na vipodozi(TFDA) kanda ya nyanda za juu kusini imezifunga machinjio mbili Mkoani Mbeya kutokana na kuwa na kasoro za kiafya.


Machinjio hizo ni Uyole iliyopo Jijini Mbeya na Mbalizi iliyopo katika Wilaya ya Mbeya Mkoani hapa kutoka na kukithiri kwa uchafu.


Kaimu Meneja wa Kanda nyanda za juu Kusini,Rodney Alananga, alithibitisha kufungiwa kwa machinjio hizo na kwamba sababu za kufunga machinjio ya Uyole Jijini Mbeya ni kutokana na  kutokuwa na miundo mbinu mizuri ya maji hivyo kuhatarisha afya za walaji na wakazi walio kando ya machinjio.


Alananga amebainisha kuwa machinjio hiyo haina uzio na kufanya watu wasiohusika kuingia machinjioni kinyume na sheria kwani watu wanaopaswa kuingia ndani ya machinjio ni wahusika tu.


Alisema  kabla ya kufunga machinjio hayo ya Uyole mara kadhaa waliongea na uongozi wa Jiji la Mbeya lakini hawakutekeleza maagizo waliyopewa mara kwa mara na hivyo Mamlaka kuamua kuifunga ili kuokoa afya za wananchi wasikumbwe na magonjwa kama kuhara na kipindupindu.


Alisema sababu nyingine ni kujaa kwa mashimo ya maji machafu kutokana na kutokunyonywa kwa muda mrefu hali inayosababisha harufu mbaya eneo hilo na maeneo yanayozunguka na kuleta uchafuzi wa mazingira Jijini.


Kwa upande wa Machinjio ya Mbalizi, Alananga alisema sababu za kufunga  ni pamoja na wafanyakazi wa Halmashauri kutokuwa na sare za kufanyia kazi kama viatu vyeupe,kofia na makoti meupe kama sheria inavyoagiza.


Alisema kuwa hali ni mbaya zaidi katika machinjio hiyo kutokana na mashimo kujaa kwa muda mrefu hivyo maji machafu na taka kufurika na kutiririsha uchafu mto Mbalizi na kuwafanya wananchi wanaotumia maji ya mto huo kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa kutokana na  wengine huyatumia kunywa kutokana na uhaba wa maji ya bomba bonde la Mbalizi.


Kutokana na  hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Magreth Akilimali, alilazimika kutembelea na kujionea hali halisi ya uchafu uliokithiri na kuahidi kuwa watafanya usafi eneo hilo kwa muda wa siku tano kuanzia Desemba 14 kwa kutumia gari la kunyonya maji machafu la Halmashauri ya Jiji la Mbeya.


Hata hivyo Akilimali,  alipoulizwa  sababu za kufungwa Machinjio hakuwa tayari kuongea eneo la tukio na kudai kuwa afuatwe ofisini kwake ambapo aliamua kuingia katika gari lake na kuondoka eneo la tukio.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa machinjio ya Mbalizi, Simon Petro(Mwadada) alisema amesikitishwa na kitendo cha kufungwa kwani kitendo hicho kimewatia hasara kubwa kwa madai kuwa itawalazimu kutumia zaidi ya shilingi elfu sitini kwenda kuchinja machinjio ya Mjini au Songwe.

Baadhi ya wafanya biashara ya nyama eneo la Mbalizi akiwemo Sikujua Mwambambe ameishukia Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutofanya usafi licha ya Madaktari wa mifugo kupima nyama kila siku na kukusanya ushuru hali inayoonesha kuna hali ya uzembe na uwajibikaji hafifu kutokana na  taarifa zimepelekwa ofisini lakini hakuna utekelezaji wowote.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya, Anderson Kabenga, amekiri kufungwa kwa machinjio hiyo na kwamba amemwagiza Mkurugenzi kufanya zoezi la usafi haraka ili kuondoa usumbufu kwa wakazi wa Mbalizi na kitendo hicho kinaipunguzia mapato Halmashauri.


Kabenga alisema wanatafuta machinjio mbadala ili huduma za uchinjaji ziendelee katika kipindi hiki cha ukarabati.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TFDA kanda ya nyanda za juu Kusini, Alananga alisema  zoezi hilo ni kutekeleza sheria ya chakula,Dawa na vipodozi sheria namba 41,43 na 44 ya mwaka 2003 na kwamba Mamlaka itaendelea kufanya ukaguzi katika maeneo mengine.


Mamlaka hiyo kwa siku za hivi karibuni imeteketeza vyakula,dawa na vipodozi hatari vilivyokwisha muda wake na vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria katika wilaya za Momba,Kyela na Jijini Mbeya.

Na Mbeya yetu

RAIS JAKAYA KIKWETE AELEKEA NCHINI MAREKANI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE.


 Rais Jakaya Kikwete
----
 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA  
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013

WATU 4 WATIWA MBARONI MKOANI KILIMANJARO KWA TUHUMA ZA KUSHIRIKI KATIKA MATUKIO MBALI MBALI YA UHALIFU NA UNYANGAJI WAKUTUMIA SILAHA


 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha Vocha za mitandao mbalimbali walizokutwa nazo watu hao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha bunduki aina ya Shotgun waliyokutwa nao watu hao.
  Vifaa mbalimbali vya kubomolea.
 Laptop mbili pia zilikuwa ni miongoni mwa vitu walivyokutwa navyo.
 Afisa wa polisi katika ofisi ya kamanda wa polisi akipanga vitu mbalimbali walivyokutwa navyo watu hao wanaotuhimiwa kuwa majambazi.
---
 Na Dixon Busagaga-Globu ya Jamii Moshi 
 JESHI la polisi mkoani Kilimanaro, limewatia mbaroni watu 4 kwa tuhuma za kushiriki katika matukio mbali mbali ya uhalifu na unyangaji wakutumia silaha yaliyotokea mkoani hapa.

Kaimu kamanda wa jeshi hilo, Koka Moita, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao baada ya kukamata gari lenye namba za usajili T564 AUW aina ya Grand Mark 2 wenye rangi ya siliva, katika maeneo ya Kiusa Manispaa ya Moshi ambalo limesadikika kushiriki kwenye matukio hayo. 

 Alisema dereva wa gari hilo ambaye alifahamika kwa jina la Nicksoni Elias Urio (28) mkaazi wa Majengo Moshi alitoa ushirikiano mkubwa ambao ulipelekea kuwakamata watu 3 ambao wamesadikika kuwa majambazi walioshiriki katika baadhi ya mtukio mkoani hapa. 
  
 “ Baada ya kuwatia mbaroni watumiwa hao, operatini kali ilifanyika yakuwapekuwa na kubaini vitu mbali mbali ikiwemo ikiwemo bumbuki aina ya shotgun ikiwa imekatwa mtutu na kitako cha bunduki hiyo hivyo hatukupata namba zake”alisema na kuendelea kuwa “laptop, 2 aina ya dell na hp, Plate namba 3 na funguo za magari, simu 8 za mkononi , vocha za simu za mitandao yote , ambaye thamani yake haijatulikana, pamoja na vifaa mbali mbali vya kuvunjia”alisema Moita.

 Moita alisema Vocha za simu bado hazijajulikana thamani yake, na uchunguzi unaendelea marautakapokamilisha watuhumiwa watafikshwamahakamani. Aidha Kamanda Moita aliwataka wananch kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufichua matukio

PRESS STATEMENT OF THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE SITUATION IN SOUTH SUDAN ISSUED BY HON. BERNARD K. MEMBE (MP), MINISTER FOR FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION DAR ES SALAAM, TANZANIA, 19TH DECEMBER, 2013


 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation
---
PRESS STATEMENT OF THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE SITUATION IN SOUTH SUDAN ISSUED BY
HON. BERNARD K. MEMBE (MP), MINISTER FOR FOREIGN AFFAIRS AND
INTERNATIONAL COOPERATION DAR ES SALAAM, TANZANIA, 19THDECEMBER, 2013
The Government of the United Republic of Tanzania is gravely concern with the deteriorating security situation in South Sudan, following the outbreak of fighting in capital, Juba, and other areas since 15 December, 2013, which resulted in a number of causalities of soldiers as well as civilian population. The fighting is a serious political setback to South Sudan, the world’s new nation which was formed in 2011 after two decades of war. Also, the fighting is a serious setback to the progress made, so far, in the last two years of the existence of South Sudan, as a sovereign state and will lead to the suffering of the civilian populations, who had already started to enjoy peace dividend.

In this respect, the Government of the United Republic of Tanzania joins the United Nations and the African Union in urging the parties concerned with the fighting in South Sudan to exercise restraint and refrain from any action that may further escalate violence, causalities and humanitarian crisis in that country.

Furthermore, the Government of Tanzania also calls upon the parties concerned to engage in dialogue in order to find a solution of their differences through peaceful means, with due respect of rule of law, human rights and constitutional legality.

Moreover, while reports indicate that so far no Tanzanian has been affected by the fighting, the Government of the United Republic of Tanzania calls upon all the parties concerned, most particularly the Government of the Republic of South Sudan to ensure the safety of all the people, not only the South Sudanese but also all the foreigners in South Sudan, including Tanzanian Nationals.

Finally, the Government of the United Republic of Tanzania wishes to express its readiness to support efforts by the United Nations, the African Union and the International Community, as a whole, aimed at finding a lasting peace to in South Sudan.

MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND
INTERNATIONAL COOPERATION

TUME YA KATIBA KUKABIDHI RASIMU YA KATIBA KWA MHE. RAIS DESEMBA 30 2013

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida. 
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye. 

Imetolewa na:
Assaa Rashid, 
Katibu, 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
Dar es Salaam, 
Alhamisi, Desemba 19, 2013

Wednesday, 18 December 2013

Binti Afariki baada ya kukutana na rafiki wa facebook ,Chukua tahadhari .

Majanga ya Facebook, Chukua tahadhari 
 Wito umetolewa angalieni marafiki mnaokutana nao katika 
mitandao,
 hasa facebook itawamaliza wanawake.Soma majanga hayo.
 
Mwanafunzi mmoja wa Shahada ya Sheria kutoka Abuja amefikwa
 na Umauti 
baada ya kula kinachosadikiwa kuwa sumu. Imeelezwa kuwa binti 
huyo
 alitoka chuoni na akamuaga room mate wake kwamba anakwenda 
kukutana na jamaa ambaye walikuwa wana chat kupitia facebook, 
ingawa alikatazwa lakini aliamua kwenda tu.

Asubuhi yake ndo mwili ukagundulika ukiwa umetelekezwa
 barabarani.




RICH MAVOKO ALIZWA NA STORY YA MAMA SHARO MILIONEA.

Na Shakoor Jongo

STORI kuhusu maisha ya mama mzazi wa staa wa komedi Bongo, marehemu Husein Mkiety ‘Sharo Milionea’, baada ya kifo cha mwanaye huyo imemliza Rich Mavoko ambaye alikwenda kumtembelea nyumbani kwake kijijini Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
Rich Mavoko akifuta machozi alipomtembelea Mama Sharo Milionea.
Akiteta machache na Risasi Vibes, Mavoko alisema, yeye kama msanii aliguswa kwenda kumsalimia mama Sharo kwa kuwa wote ni wasanii na aliona mama huyo anahitaji faraja kutoka kwa watu waliokuwa karibu na mwanaye.
“Mama alifurahi sana kuniona. Tulizungumza mengi lakini niliguswa sana na matatizo aliyonayo mama yetu. Mama anasema, mali nyingi za marehemu mwanaye, amekuwa akizisikia tu lakini hajapewa.
Mavoko na Mama Sharo wakiwa katika kaburi la Marehemu Sharo Milionea.
“Kiukweli mama Sharo anatia huruma sana kwani faraja imepotea, mali za mwanaye hazioni, amebaki akitia huruma.
Unajua marehemu alikuwa akimsadia sana mama yake, ndiyo lilikuwa tegemeo lake kubwa. Ameondoka na kumuacha akiwa hana la kufanya, mbaya zaidi hata mali zake ambazo zingepaswa kumsaidia kipindi hiki, wajanja wamezidhulumu.
“Dunia haina usawa kabisa. Kiukweli inatia huruma sana. Nawasihi wasanii wenzangu na wadau wa sanaa, inatakiwa tukumbuke wenzetu waliotangulia tena kwa kuwaenzi kwa kila njia.
Marehemu Sharo Milionea enzi za uhai wake.
Kuna vitu vinauma sana amenieleza tangu kifo cha mwanaye haki zake nyingi hajui zilipo. Tuungane wasanii tuwasaidie wazazi wa wasanii wanaotangulia mbele za haki,” alisema Mavoko.RICH

DUH! HOMA YA MPAMBANO WA MSONDO, SIKINDE WAZIDI KUPANDA.


Sikinde yajichimbia Bagamoyo

Na Badru Kimwaga
HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.

Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.

Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.
Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.
"Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.

Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.

ZAIDI YA WATU 200 WALIOKUWA WAKISAFIRI KWA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUTUA DHARURA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA.

Watu 200 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Ethiopian Airline wanusurika kufa baada ya ndege kupitiliza hadi nje ya uwanja mdogo wa ndege wa Arusha baada ya kutua kwa dharura.
Muonekano wa ndege ya Ethiopian Airline baada ya kutua kwa dharura.