TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday, 30 April 2016

How children learn to read and write

When adults write, we do so for a real reason: to write a shopping list, to leave a note for someone, to fill in forms, to communicate with a friend in a letter or email, to create a story. Children learn to write most easily when they write for real reasons too rather than because an adult has told them what they should write about.
Like all other things worth learning how to do, learning to write is a process. We can help our children develop their skills at writing by understanding where they are in their development and encouraging them.
Drawing as a first step
  • Drawing and painting are useful ways for young children to express their ideas and feelings. They need lots of opportunities to do this. You can help young children understand the connection between drawing and writing by asking them to talk about their pictures and then later on, asking what they would like you to write about their pictures. You can write about their picture under it. This helps them to understand that written language has meaning.
  • Encourage them to use writing in the fantasy games by making sure that writing and drawing materials are available. For example, in the game ‘shop-shop’, leaving a notepad and pencil around encourages them to ‘write’ a shopping list.
  • Ask children to draw a picture about a story they have heard or to draw their favourite part of a story you have read together.
Early writing
When children realise that writing communicates meaning, they begin to experiment with it. They use writing for different real purposes in their lives. Most commonly they:
  • Try to write their name
  • Write to label things in their pictures
  • Use writing to organise different parts of their daily lives – for example: writing a list of children coming to a birthday party, or of the things they would like for their birthday or another occasion
  • Write to communicate messages to important people in their lives
  • Write to imitate the ways that adults in their lives use writing – for example: filling in forms or competition entry forms.
When children first start to write they usually use scribbles on a page. From here children often begin to use symbols that look more like letters and then they start to use real letters (even though they may be back to front sometimes!) together with their own symbols. These are exciting first steps because they show that children are aware of a difference between drawing and writing.  You can support their attempts at writing by asking them what the writing says.
Using conventional writing
Next children start writing in words, using the letters of conventional writing. They usually choose letters that they think match the sounds in words they are trying to write. Through experimenting, they gradually become more aware of how we write from the top of the page to the bottom, and from left to right and also how numbers are different to letters.
Encourage children’s writing by reading it aloud or asking them to do so, displaying it around your home (for example, on the fridge) and by writing back to them!
Over time, as children are exposed to examples of writing in their environment and in books you read with them, they gradually incorporate the use of punctuation in their writing and use conventional spelling more and more. They even begin to pick up ‘mistakes’ in their own writing and rewrite words or letters. While they start out writing mainly to record and communicate messages, if you keep reading with them, you will find they begin to write their own simple stories!

Wednesday, 19 August 2015

Kongamano la wajasiriamali kufanyika Mwanza September 26, 2015.

Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza  Ukumbi wa  Benki Kuu (BoT), Capripoint.
Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI  zaidi ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika kongamano la mafunzo ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.

Akizungumza na Dar es Salaam leo, Mratibu wa kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.

"Wajasiriamali hao katika kongamano hilo watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza mitaji yao na mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.

Alisema makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia wajasiriamali hao kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza wa bidhaa zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.

Alisema mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika shughuli za ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya  makongamano hayo yamewanufaisha wajasiriamali  wengi.

Kilyabusebu alisema kongamano hilo lililoandaliwa na  Jumuiya ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Business Entrepreneurs Women) litafanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza  katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) Capripoint.

Mratibu huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila mshiriki atalazimika kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo ambapo katika mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia bidhaa na kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.


Kilyabusebu alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa kanda ya ziwa kuweza kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza stadi za kazi zao.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba  0754032589 /0756334078/0673032589.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

Sunday, 16 August 2015

Kongamano la wajasiriamali kufanyika Mwanza tarehe 26/09/2015 katika ukumbi wa BOT



Jumuiya ya Wanawake wajasiriamali Tanzania (Tanzania Business Entrepreneurs Women) inakuletea kongamano la wajasiriamali litakalofanyika mkoani MWANZA, tarehe 06/09/2015 katika ukumbi wa benki kuu capripoint(B. O. T) ,kongamano hilo litashirikisha wajasiriamali mbali mbali watakaouza na kutangaza bidhaa zao.  Pia kutakuwa na mafunzo ya namna ya kukuza mtaji mdogo na mbinu nyingi za kukuza biashara yako. Wajasiriamali wote wanakaribishwa ambapo kiingilio kitakuwa:
Mafunzo pekee na chakula sh.30,000,
Meza ya kuuza bidhaa pekee sh.20,000,
Mafunzo na Meza sh. 50,000,
Kwa mawasiliano zaidi tupigie namba. 0754032589/ 0756334078/ 0673032589.

WOTE MNAKARIBISHWA.

Monday, 29 June 2015

KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS WOMAN) LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden Dar es Salaam.
 
 Wadau wa kongamano hilo wakiwa wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth Mjale.
 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba 
akitoa mada.
 Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo. 
 Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa  kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa.
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea.

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
  Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.

"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale

Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.

Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)