TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Tuesday, 21 October 2014

Ratiba ya CCM ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa

RATIBA YA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA
SERIKALI ZA MITAA NDANI YA CHAMA


TAREHE
 SHUGHULI
19/10/2014 -  22/10/2014
Mikutano ya Wanachama wote wa CCM Matawini kwa ajili ya kuelimishwa na kuhamasishwa kuhusu Uchaguzi.
23/10/2014 – 25/10/2014
Kuchukua na kurejesha Fomu za kuomba kugombea Uenyekiti wa Mtaa, Kijiji, Kitongoji na Ujumbewa Serikali za Vijiji na Mitaa kwa Makatibu wa Matawi ya CCM.
26/10/2014 – 27/10/2014
Kampeni ya wagombea ndani ya Chama.
28/10/2014 – 29/10/2014
Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kitongoji na Wajumbe wa Kamati ya Kitongoji kwenye Mashina yanayohusika.
 30/10/2014 – 31/10/2014
Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wa  Halmashauri ya Kijiji na vilevile kupiga kura za Maoni kwa Wagombea Uenyekiti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa kwa Mijini.  Kura zitapigwa na wanachama wote wa CCM kwenye Matawi ya Kijiji au Mtaa husika.
01/11/2014 – 03/11/2014
Kamati za Siasa za Matawi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Kata
04/11/2014 – 06/11/2014
Kamati za Siasa za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Kata na kwa Kamati za Siasa za Wilaya.
07/11/2014 – 09/11/2014
Halmashauri Kuu za Kata kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea Uenyekiti wa Vitongoji.
10/11/2014 – 11/11/2014
Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Wilaya.
12/11/2014 – 14/11/2014
Halmashauri Kuu za Wilaya kufanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea Uenyekiti wa Mtaa, Uenyekiti wa Vijiji, Wajumbe wa Kamati za Mitaa na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji.
15/11/2014 – 21/11/2014
Kuchukua Fomu na kurudisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
16/11/2014 – 21/11/2014  
Mafunzo ya wajibu wa Wagombea na Mawakala.
24/11/2014
Siku ya uteuzi wa Wagombea kwa Msimamizi.

No comments:

Post a Comment