TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Saturday, 18 October 2014

NANI MTANI JEMBE?SIMBA WAIBUKA KIDEDEA LEO ASUBUHI ZIDI YA WATANI WAO YANGA.

Leo katika viwanja vya shule ya msingi Kijitonyama Watani wamemenyana vikali, ambapo Simba kuibuka kidedea kwa Penarty zidi ya  Yanga.Shindano hilo limefanyika ambapo Mshindi wa kwanza kaibuka na zawadi ya Mbuzi na pesa tasilimu Shilingi 150,000.Mshindi wa pili kaibuka na Mbuzi mdogo na pesa tasilimu shiling 50,000. Na mwandishi wetu(http://www.nkema.blogspot.com/)













 Mchezaji wa Yanga akipiga Penarty

 Mchezaji wa Simba akipiga Penarty.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia Ushindi zidi ya mahasimu wao Yanga.




 Simba katika picha ya Pamoja.

Diwani kata ya Kijitonyama akiwapongeaza wachezaji kwa kufanya vizuri katika mchezo huo.
 Washindi wa Kwanza (Simba) wakipokea zawadi


Diwani wa Kata ya Kijitonyama akimkabidhi Nahodha wa Simba, Mshindi wa kwanza mtani Jembe Zawadi ya Mbuzi pamoja na pesa tasilimu 150,000 ikiambatana na Mpira.




Diwani wa Kata ya Kijitonyama akimkabidhi Nahodha wa timu ya Yanga, Mshindi wa pili mtani Jembe Zawadi ya Mbuzi pamoja na pesa tasilimu50,000 ikiambatana na Mpira.

Yanga katika picha ya pamoja.

Mechi hiyo ilichezwa Leo ambapo dakika 90 timu zote zilitoka sare ya goli moja kwa moja, Ambapo dakika za mwanzo Montego Frank aliipatia Yanga bao, kipindi cha pili dakika ya 90 Zicco aliipatia Simba bao. Penarty zilipigwa na Kutoka Yanga wapigaji walikuwa Bakari kikuji,Kelvine Gawasa,Ben Kalenga,Kulwa Ndege na Ibrahimu Mwalami. Ambapo penarty za Simba zilipigwa na Rashid Ismail,Rama Mzee,Ally Hassan,Ngwesa na Zicco.

No comments:

Post a Comment