Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa
Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi Florence Kasenene cheti
cha ushiriki katika promosheni ya Weka na Ushinde katika hafla
iliyofanyika viwanja vya benki hiyo Tawi la Sinza Mori Dar esaSalaam leo
asubuhi. Kasenene alijishindia bajaj.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi funguo wa bajaj, Florence Kasenene katika hafla hiyo.
Ofisa Habari wa benki hiyo, Doris (kushoto), akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Mshindi wa pikipiki, Mariam Mburinyingi akifurahi kushinda pikipiki hiyo na mmoja wa maofisa wa benki hiyo.
Mshindi wa baiskeli, akiijaribu kuiendesha baada
ya kukabidhiwa.
Washindi wa baiskeli wakiwa na baiskeli zao pamoja
na maofisa wa benki hiyo.
Baiskeli walizokabidhiwa washindi.
Pikipiki walizokabidhiwa washindi hao.
Bajaj na pikipiki zilizokabidhiwa kwa washindi.
BENKI ya NMB imetoa zawadi za pikipiki,
bajaj na baiskeli kwa washindi wa promosheni ya Weka na Ushinde
inayoendeshwa na benki hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB,
BENKI YA NMB YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDI
Salie Mray alisema washindi waliopata zawadi kwa mwezi wa kwanza wa promosheni hiyo ni wa Kanda ya Dar es Salaam.
"Kwa Kanda ya Dar es Salaam tuna
washindi 30 ambao zawadi zao tunawakabidhi leo 'jana' na wale wa Kanda
zingine watapewa zawadi zao kwenye kanda zao" alisema Mray.
Aliwataja washindi walioshinda bajaj ni
watano, washindi watatu wameshinda pikipiki za magurudumu mawili na
washindi 22 wamejishindia baiskeli aina ya Phoenix.
Alisema katika promosheni hiyo kuna
zawadi nyingi za kushindania zenye thamani ya sh.milioni 500 hivyo
watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani droo zingine zitaendelea
kuchezeshwa kila Jumatatu.
Alisema zawadi zilizotolewa jana
zinatokana na droo ya nne iliyofanyika kwa nchi nzima ambapo tayari
wamepatikana washindi wa 17 wa bajaj, 16 pikipiki na 132 baiskeli aina
ya Phoenix.
Mray alisema hiyo ni fursa kwa wateja
wao kwani kila mtu anaweza kushinda ili mradi tu afuate taratibu za
kushiriki ambazo ni kuweka fedha kwenye akaunti yake mara nyingi
awezavyo ili kujiongezea naafasi zaidi kushinda. (Imeandaliwa na mtandao wa http://nkema.blogspot.com/-simu namba 0754-032589)
No comments:
Post a Comment