TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Friday, 13 December 2013

MAMA MMOJA AMWAGIWA MAJI YA MOTO MWILI MZIMA KISA MAPENZI


Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili zima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA
 Na Gadiola Emanuel -Arusha

Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.


Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi


Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema
majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini
hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la
madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru
Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo  yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini

Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza
wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia
katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza  swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo   hayo.

Maria Maswa-Afisa Dawati  la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza  kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog.

No comments:

Post a Comment