TAFUTA CHOCHOTE NDANI YA NKEMA

Monday, 14 October 2013

MAKUMBUSHO YA KUMBUKIZI YA NYUMBA YA MWL NYERERE ILIYOPO MAGOMENI MTAA WA IFUNDA YATEMBELEWA NA WAKAZI WA DAR ISHARA YA KUADHIMISHA SIKU YA MWL NYERERE TOKEA KUFARIKI KWAKE MAPEMA LEO



 
 Bango linalosomeka Nje ya Nyumba ya Kwanza aliyowahi kuishi Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda barabara ya ifunda 60
 Hii ndio nyumba aliyoishi Hayati Baba Wa Taifa Mwl Julius Nyerere Kwa Kipindi Cha Miezi nane iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda, Barabara ya Ifunda namba 60 ambayo sasa imekuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Nyumba ya Mwl Nyerere
 Baadhi ya Wakazi wa Jiji La Dar Wakiwasili kwenye Nyumba aliyokuwa anaishi Hayati Mwl Nyerere Kipindi hiko kwaajili ya kujifunza na kufahamu historia yake japo kwa kifupi
 Wakazi wa Jiji la Dar Wakipata Maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu (hayupo pichani) wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakati walipofika leo kutembelea nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Hayati Baba wa taifa Mwl Julius Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa ifunda
 Mmoja wa Kijana aliyefika kwaajili ya Kutembelea Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaani wa Ifunda Jijini Dar akiandika jina katika kitabu cha Wageni  mapema leo wakati alipotembelea Nyumba Hiyo leo
 Wakazi wa Jiji la Dar wakionyeshwa Chumba cha Watoto wa Kiume wa Hayati Baba Wa Taifa Mwl Juilus Nyerere na mmoja wa wahudumu wa Nyumba hiyo (hayupo pichani) wakati waliotembelea makumbusho ya kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere mapema leo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Jijini Dar
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo ya Redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere kama zawadi na Malkia Elizabeth kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha wakazi wa jiji la Dar waliofika katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda 
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha Rozari aliyokuwa akitumia Hayati baba wa Taifa Mwl julius Kambarage Nyerere 
 Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat Lukaza pamoja na Wakazi wengine wakipata maelezo kutoka kwa Bi Theresia Gratta Makene (katikati) juu ya redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere Kama Zawadi kutoka Kwa Malkia Elizabeth 
 Wakazi wa Jiji la Dar wakiangalia baadhi ya Picha zilizobandikwa katika Kuta za Nyumba aliyokuwa akiishi Hayati Mwl Nyerere Kwa kipindi cha Miezi nane, Nyumba hiyo ipo Magomeni Mtaa wa Ifunda
 Baadhi ya watoto waliofika Katika nyumba hiyo Kwaajili ya Kuona vitu mbalimbali alivyowahi kutumia Hayati Mwl Nyerere vilivyopo katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda
 Watoto waliofika mapema leo Katika Nyumba aliyowahi kuishi Hayati Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakiangalia vitabu vya Mwl Nyerere
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akielezea juu ya baadhi ya vyombo alivyowahi kutumia Hayati baba wa taifa Mwl Nyerere wakati akiishi katika nyumba hiyo iliyopo Magomeni mtaa wa Ifunda.

No comments:

Post a Comment